Video : DIVASHINE ametusogezea Video yake mpya "KILA SAA" hembu itazame alafu mdondoshee comment hapo chini

Divahine ni msanii chipukizi anaekuja kwa kasi katika tasnia hii ya music , anaetamba ya kibao chake cha "MBELE KWA MBELE;" sahivi ametuletea Ngoma nyingine kali sana inaitwa "KILA SAA' , Hembu itazame hapo chini alafu acha comment kama vipi ,
Kama uliikosa kuitazama video yake ya "Mbele kwa mbele " basi itazame hapo chini



Maneno ya RC Makonda kuhusu wafanyakazi hewa Dar es Salaam…

April 20 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda alikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia headlines za wafanyakazi hewa katika mkoa wake pamoja na hatua zinazochukulia kuwafikisha katika vyombo husika.
Katika mkutano huo RC Makonda alisema….’Mara ya kwanza tulipata idadi ya watu 71 nikaomba muda ukasogezwa mbele na Mh.waziri Simbachawene tumeendelea kufanya utafiti tukagundua idadi inaongezeka maana sasa lakini kadri tunavyozidi kufanya utafiti idadi inaongezeka maana yake sasa kuna uwezekano mkubwa tukatoa takwimu sio sahihi’ RC Paul Makonda
Kwasababu kila unapokaa kidogo tunajikuta tunapata taarifa tofauti kwahiyo tumeona ngoja tujulishe umma kwamba hatua tunazoanza kuzifanya moja nimeelekeza wakuu wote wa wilaya kuacha kufanya shughuli yoyote na kulisimamia zoezi hili kuhakikisha kila mtu anaenda sekta kwa sekta kubaini watu hao ‘ – RC Paul Makonda
Lakini suala la pili tumeongea na wizara uhusika tumefanya mazungumzo na wizara ya utumishi na wizara ya ofisi ya Rais na utawala bora ili kupata nguvu ya utaalamu zaidi ili tuweze kuwabaini wahusika hao lakini jambo lingine kwenye wilaya ya kinondoni watu 34 tayari wameshafunguliwa majalada kwa maana nyingine kwamba tumeshawaripoti katika vyombo husika na ukienda unaweza ukapata kumbukumbu namba 240282/0.1d/26 ya tarehe 8 mwezi huu inaongea suala hilo’ – Rc Paul Makonda

(+Video) Waziri Nape na Rc Makonda walivyoungana na wananchi kumuaga Ndanda Kosovo Dar..

April 9 2016 muziki wa dance ulipata pigo baada ya  kuondokewa na mkali wa muziki wa dance Tanzania Ndanda Kosovo ambaye alifariki akiwa kwenye matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es salaam
hatimaye April 13, mazishi yamefanyika katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam, Na kuhudhuriwa na watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa Nchi kama vile Waziri wa Habari, utamaduni sanaa na Michezo Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda.
Wasanii kadhaa pia walijitokeza kutoa heshima za mwisho kumsindikiza mwenzao.

VIDEO: Diamond karudi Tanzania… kayaongea haya kuhusu Fally Ipupa, Awilo na mengine

Diamond Platnumz amemaliza kufanya show zake kwenye miji tisa ya Ulaya na sasa amerudi nyumbani Tanzania kwa ajili ya kuendelea na harakati nyingine…. wakati anatua Airport Dar es salaam AyoTV ilimpata kwenye Interview hii hapa chini.


sababu zilizoondoa Ukuu wa Mkoa wa Anne Kilango Malecela

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anne Kilango Malecela na Katibu Tawala wa Mkoa huo Abdul Rashid Dachi, kufuatia mkoa huo kutoa taarifa zisizo sahihi kuwa hauna watumishi hewa.
Rais Magufuli ametangaza kutengua uteuzi wa Viongozi hao wa Mkoa wa Shinyanga leo April 11 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam, mara baada ya kupokea Taarifa ya Mwaka 2014/2015 ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), na kupokea hundi kifani ya shilingi Bilioni 6 kutoka Ofisi ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zilizotokana na kubana matumizi.
Rais Magufuli ameeleza kuwa baada ya kupata taarifa kuwa Mkoa wa Shinyanga hauna watumishi hewa, aliamua kutuma timu ya ukaguzi iliyokwenda kufanya uchunguzi ambapo hadi kufikia jana Aprili, 10 2016 imebaini kuwepo watumishi hewa 45 huku zoezi likiwa linaendelea katika wilaya mbili za Ushetu na Shinyanga Vijijini.
>>>’Na wale wote wa Shinyanga ambao walisemekana ni zero, hakuna mtumishi hewa, walikuwa tayari wameshalipwa shilingi milioni 339.9, nimejiuliza sana, na nikajiuliza sana na kwa kweli nimejiuliza sana na kwa masikitiko makubwa, kwa nini Mkuu wa Mkoa alisema hakuna mtumishi hewa?’:-Rais Magufuli
Rais Magufuli amesema baada ya kutengua uteuzi wake, Anne Kilango Malecela atapangiwa kazi nyingine.
Pamoja na hatua hiyo, Rais Magufuli ametaka wakuu wa mikoa yote wawafichue watumishi hewa wote ili waondolewe mara moja, na ameagiza timu iliyofanya uchunguzi Mkoani Shinyanga itumike kufanya uchunguzi katika mikoa mingine kwa lengo la kukomesha upotevu mkubwa wa fedha za umma.
Katikati ya Mwezi Machi, 2016 Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa yote nchini kusimamia zoezi la kuwaondoa watumishi hewa wote katika orodha ya malipo ya mshahara, ambapo mpaka tarehe 31 Machi, 2016 Jumla watumishi hewa 5,507 walibanika.
Kati ya shilingi Bilioni 583 ambazo serikali imekuwa ikitumia kila mwezi kwa ajili kulipa mishahara, kati ya shilingi Bilioni 53 na 54 zimekuwa zikipotea kutokana na kulipa mishahara ya watumishi hewa.

KRC Genk ya Samatta imeibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya KV Oostende, hili ndio goli la Samatta (+Video)

Headlines za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania ambaye pia ni nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta kuzidi kufanya vizuri zinazidi kuongezeka kila kukicha ndani ya Ligi Kuu Ubelgiji akiichezea klabu ya KRC Genk.
Samatta amerudi kwenye headlines baada ya kocha wa klabu ya KRC Genk kumpa nafasi ya kucheza mechi dhidi ya KV Oostende. KRC Genk imeibuka na ushindi wa goli 4-0, lakini kama kawaida Mbwana Samatta alifunga goli la tatu la Genk dakika ya 77 baada ya kuingia dakika ya 77 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.
Goli la Samatta lilifungwa baada ya Samatta kutumia vyema pasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Neeskens Kebano. Goli hilo linakuwa goli la tatu kwa Samatta toka ajiunge na klabu ya KRC Genk.
Video ya goli la Samatta

Je ni kweli Diamond Platnumz katoboa pua?! ukweli ninao hapa

Kwa saa kadhaa zimeenea taarifa za mwimbaji staa wa bongofleva Diamond Platnumz kuonekana katoboa pua, hii habari imepewa nguvu kutokana na picha aliyoipost Diamond mwenyewe kwenye Instagram akionekana katoboa pua.
Ukweli ukoje? …ukweli ni kwamba Diamond hajatoboa pua kama wengi walivyodhani ambapo Meneja wake aitwae Sallam aliwajibu hivi mashabiki walioanza kuuliza >>> ‘Usiamini kila unachoona kwenye picha au unachoambiwa, mlikuwa mmelala sana amewaamsha kidogo’


Disqus Shortname

Comments system