Samatta amerudi kwenye headlines baada ya kocha wa klabu ya KRC Genk kumpa nafasi ya kucheza mechi dhidi ya KV Oostende. KRC Genk imeibuka na ushindi wa goli 4-0, lakini kama kawaida Mbwana Samatta alifunga goli la tatu la Genk dakika ya 77 baada ya kuingia dakika ya 77 kuchukua nafasi ya Nikolaos Karelis.
Goli la Samatta lilifungwa baada ya Samatta kutumia vyema pasi ya mshambuliaji wa kimataifa wa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo Neeskens Kebano. Goli hilo linakuwa goli la tatu kwa Samatta toka ajiunge na klabu ya KRC Genk.
Video ya goli la Samatta