Harmonize azungumza kuhusu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Huddah
Harmonizealikanusha kuwepo kwa mahusiano yake na mwanadada huyo
japokuwa walisha wahi kukutana katika harakati za kufanya kazi lakini
hawana mahusiano ya kimapenzi. Amesema kuwa Huddah ni miongoni mwa wanawake wazuri lakini sio kweli kuwa wanamahusiano ya kimapenzi bali wana project ya pamoja ambayo wanatarajia kuifanya siku za karibuni.
Lakini kipindi cha nyuma wawili hawa walionekana kwenye video ya pamoja wakiwa wanapigana mabusu huku Huddah akionyesha na kusema anahisi aibu.