Leo March
18 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi
kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea
mwenendo wa jeshi hilo, lakini kubwa ni hili la kutangaza kutoa zawadi
ya milioni moja kila baad ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi
aliyepambana na majambazi.
‘Askari
wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa,
lakini nimeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na
Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya
vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake
kama motisha‘ ;-Paul Makonda
‘Kuna
watu wengi wana silaha halali na wawengine wanamiliki isivyo halali,
kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba
wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za
uhalali wa silaha zao, tunataka kujihakikishia tunzao silaha ngapi
katika mkoa wetu kwamaana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu’ ;-Paul Makonda
‘Sasa
olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar
es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye
mabenki wala kuwapora watu kwa silaha‘ ;-Paul Makonda
Ilikupita hii Video ya Agizo la kwanza alilolitoa Paul Makonda kama mkuu wa mkoa?