Harmonize ataja sababu ya kumshirikisha Diamond Platnumz kwenye ngoma ya 'Bado'

 Mkali wa wimbo wa ‘Aiyola’ na ‘Kidonda Changu’, Harmonize, amezidi kumng’ang’ania mkali wa Bongo Fleva Afrika Mashariki, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kuendelea kumshirikisha katika wimbo wake mpya wa ‘Bado’.

Harmonize alisema ameamua kumshirikisha mkali huyo kutokana na maoni ya mashabiki wao kufananisha uimbaji wao, hivyo wameamua kuimba pamoja ili mashabiki wao waone utofauti wao.

Beat ya wimbo huo imetengenezwa na prodyuza Fraga ambaye awali alimtumia midundo mitatu tofauti akachagua huo.

Pia video ya wimbo huu imefanyika nchini Afrika Kusini na muongozaji ni Nick, aliyeongoza video ya Aiyola ya Harmonize, ‘Make Me Sing’ ya Aka na Diamond, ‘Love Boat’ ya Kcee na Diamond na ‘Walk it off’ ya Fid Q.
TAZAMA VIDEO

                   AUDIO YAKE HII HAPA
Downloading Mp3 audio

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

Disqus Shortname

Comments system