April 20 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda
alikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia headlines za
wafanyakazi hewa katika mkoa wake pamoja na hatua zinazochukulia
kuwafikisha katika vyombo husika.
Katika mkutano huo RC Makonda alisema….’Mara
ya kwanza tulipata idadi ya watu 71 nikaomba muda ukasogezwa mbele na
Mh.waziri Simbachawene tumeendelea kufanya utafiti tukagundua idadi
inaongezeka maana sasa lakini kadri tunavyozidi kufanya utafiti idadi
inaongezeka maana yake sasa kuna uwezekano mkubwa tukatoa takwimu sio
sahihi’ – RC Paul Makonda
‘Kwasababu
kila unapokaa kidogo tunajikuta tunapata taarifa tofauti kwahiyo
tumeona ngoja tujulishe umma kwamba hatua tunazoanza kuzifanya moja
nimeelekeza wakuu wote wa wilaya kuacha kufanya shughuli yoyote na
kulisimamia zoezi hili kuhakikisha kila mtu anaenda sekta kwa sekta
kubaini watu hao ‘ – RC Paul Makonda
‘Lakini
suala la pili tumeongea na wizara uhusika tumefanya mazungumzo na
wizara ya utumishi na wizara ya ofisi ya Rais na utawala bora ili kupata
nguvu ya utaalamu zaidi ili tuweze kuwabaini wahusika hao lakini jambo
lingine kwenye wilaya ya kinondoni watu 34 tayari wameshafunguliwa
majalada kwa maana nyingine kwamba tumeshawaripoti katika vyombo husika
na ukienda unaweza ukapata kumbukumbu namba 240282/0.1d/26 ya tarehe 8
mwezi huu inaongea suala hilo’ – Rc Paul Makonda