April 9 2016muziki wa dance ulipata pigo baada ya kuondokewa na mkali wa muziki wa dance Tanzania Ndanda Kosovo ambaye alifariki akiwa kwenye matibabu katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dar es salaam hatimaye April 13, mazishi yamefanyika
katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam, Na kuhudhuriwa na watu
mbalimbali wakiwemo viongozi wa Nchi kama vile Waziri wa Habari, utamaduni sanaa na Michezo Nape Nnauye, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda. Wasanii kadhaa pia walijitokeza kutoa heshima za mwisho kumsindikiza mwenzao.