Timu ya taifa ya Brazil leo alfajiri ya
June 9 2016 ilishuka dimbani kucheza mchezo wake wa pili wa michuano ya
Copa America dhid ya timu ya taifa ya Haiti, katika mchezo huo Brazil
ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 7-1.
Brazil ambao walikuwa na wachezaji wao
nyota kasoro Neymar Junior, walianza kupata goli la kwanza kupitia kwa
Philipo Coutinho aliyefunga magoli matatu yaani hat-trick kuanzia dakika
ya 14, 29 na 90, Renato Agusto aliyefunga magoli mawili dakika ya 35 na
86, Gabriel dakika ya 59 na Lucas Lima dakika ya 57, wakati goli pekee
la Haiti lilifungwa na James Marcelin dakika ya 70.