Picha hiyo inaonesha ni jinsi gani Messi alivyo maarufu duniani na kuwagusa wengi lakini kampeni ya kuanza kumtafuta mtoto huyo ni nani ilianza mara moja kupitia mitandao ya kijamii.
Picha hiyo ilianza kusambaa katikati ya mwezi January lakini baadaye ikafahamika kijana huyo alikuwa ni wa Afghanistan.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka mitano anafahamika kwa jina la Murtaza Ahmadi kutoka Afghanistan vijijini.
Jumapili website ya michezo ya Argentina TYC ilithibisha kwamba Messi amezipata picha za Murtaza na amepanga kukutana na kijana huyo.
Murtaza, ambaye anaishi Ghazni, Kusini mwa Afghanistan ameshatafutwa kwa ajili ya kukutana na Messi. Kwasasa bado haijapangwa siku wala saa ambapo pande mbili hizo zitakutana.
Afisa habari wa shirikisho la soka la Afghanistan, Syed Ali Kazemi, ametangaza kwamba: “Uongozi wa Afghan Football Federation (AFF) umepokea email kutoka kwa Lionel Messi na Barcelona kuhusu Messi kukutana na Murtaza”.
Murtaza atatimiza ndoto yake ya kukutana na Leo Messi lakini kuna taarifa inayosema kwamba kijana huyo ni shabiki mkubwa wa Cristiano Ronaldo