Saudia yamnyonga mtu wa 69 mwaka huu




Hatua ya Saudi Arabia ya kumnyonga raia mmoja wa Misri aliyehukumiwa kwa kosa la ulanguzi wa madawa ya kulevya, inafikisha idadi hadi 59 ya watu walionyongwa mwaka huu na himaya hiyo ya kiislamu.
Hayo ni kwa mjibu wa waziri wa maswala ya ndani nchini Saudi Arabia.
Taarifa ya wizara ya usalama wa ndani nchini humo na ambayo ilitangazwa katika shirika la habari la serikali SPA, zilisema kuwa, Ibrahim Mohammed Salman, alikamatwa alipokuwa akisafirisha dawa ya kulevya aina ya Opium inayotumika kutengeneza Kokain, iliyokuwa imefichwa ndani ya gari lake.
Taarifa zaidi zasema kwamba, Ibrahim Mohammed Salman alinyongwa kaatika mji wa Tabuk ulioko Kaskazini mwa nchi hiyo.
Nyingi ya hukumu ya kifo katika taifa hilo lenye sheria kali inatekelezwa kwa mhusika kukatwa shingo kwa upanga.
Januari tarehe mbili mwaka huu utawala wa Saudia uliwanyonga watu 47 waliotuhumiwa kuwa magaidi.
Kwa mjibu wa shirika la AFP, mwaka jana wa 2015, watu 153 wengi wao walanguzi wa mihadarati au wauwaji, walinyongwa.
Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International linasema kuwa idadi ya watu walionyongwa nchini Saudi Arabia mwaka jana pekee ilikuwa ya juu zaidi katika kipindi cha miongo miwili.
Aidha, takwimu hiyo ni chini ikilinganishwa na hukumu ya mauwaji yanayotekelezwa na China pamoja na Iran.


Utawala wa Saudi Arabi unatekeleza kazi yake chini ya sharia kali ya kiislamu ambapo hukumu ya kifo kwa walanguzi wa dawa za kulevya, wizi wa kutumia silaha, ubakaji na uasi .
Wakati huo huo, shirika la Human Rights Watch limemshutumu waziri wa haki na sheria kwa kutangaza "mauwaji ya halaiki" dhidi ya wanachama wa vuguvugu la kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood, ambalo tayari linakabiliwa vikali na ukatili wa msako wa polisi.
Waziri wa haki na sheria Ahmed al-Zind, alisema mwezi Januari kuwa "hataridhika hadi pale wanachama 10,000 wa kundi la Muslimu Brotherhood wameuwawa kwa kila kifo cha mwanajeshi au afisa wa polisi''.
Kundi la Human Rights Watch limemuomba rais Abdel Fattah al-Sisi kulaani matamshi hayo, likisema "linachochea hisia ya watu wengi nchini humo hasa maafisa wakuu wa serikali na wanahabari maarufu, ambao tayari wametoa matamshi makali ya kinyama dhidi ya kundi hilo la Muslim Brotherhood.
Tangu Sisi, ambaye mwenyewe alikuwa kamanda mkuu wa majeshi, kuun'goa utawala wa kiislamu wa rais Mohamed Morsi, mnamo Julai 2013, imeshuhudia polisi wa Misri wakiendesha operesheni kali ambayo imesababisha vifo vya mamia ya wanachama wa Muslim Brotherhood.
Shirika la Human Rights Watch aidha limesema kwamba Agosti 14 mwaka 2013 polisi waliwauwa takriban watu 817 waliokuwa wakifanya maandamano ya kumuunga mkono Morsi katikati mwa Cairo na kuna uwezekano mauwaji hayo yalifikia kiwango cha kuwa uhalifu dhidi ya binadamu.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

Disqus Shortname

Comments system