Mwigizaji maarufu wa Bongo Movie hapa nchini Ray Kigosi amesema kwamba yeye hajawahi kujichubua bali huwa anakunywa maji mengi pamoja na kufanya mazoezi
Ray ameyasema hayo wakati akifanya mahojiano katika kipindi cha ENews kinachorushwa na EATV na kusema kwamba hua anakwenda salon mara moja kwa wiki kwa ajili ya kusafisha uso wake (Scrub) ili akiwa anafanya kazi zake watu waweze kumwona vizuri na kupenda kazi zake.
“Zamani kipindi kile shida kuingia saloon kufanya scrub, sasa hivi najiweza katika hivyo vitu, kwa hiyo kwa kila wiki moja lazima nifanye scrub, nijitengeneze mwili wangu kama kioo cha jamii ninapotokea katika TV, basi kwanza kabla sijaanza kuzungumza wewe Mtanzania uweze kuniadmire, kwa hiyo kimsingi sijichubui, mimi nafanya sana mazoezi ndio siri ya ngozi yangu kunawiri”, alisema Ray Kigosi.
Hivi karibuni kuliibuka minong’ono na hata msanii wa muziki wa bongo fleva Nay wa Mitego, kumuimba msanii huyo wa filamu kuwa amekuwa mkongo na kubadilisha rangi yake. (Kujichubua).
Naye Mpenzi wake Chuchu Hans amesema kwamba Mpenzi wake hajichubui bali ni maisha yamemkubali tofauti na hapo nyuma alivyokuwa anahangaika kuinua sanaa na kipaji chake.
Katika kipengele cha ”Cheche” ambacho majirani hupewa nafasi ya kumzungumzia msanii au mgeni wa siku kwenye show wamesema kwamba Ray apunguze kutumia vipodozi kwani anakuwa kama mchina.
Pia wamemtaka mwigizaji huyo kuwa na moyo wa kusaidia wasanii chipukizi ilikukuza tasnia ya uigizaji hapa nchini.