Single mpya ya Vanessa Mdee ‘niroge’ tayari imepokelewa TRACE URBAN

March 28 2016 single mpya ya Niroge‘ ya mwimbaji Mtanzania Vanessa Mdee umegongwa kama starter kwenye Television ya Ufaransa Trace TV ambayo matangazo yake yamekua yakionekana Afrika, video hii mpya iliwekwa kwenye mtandao wa YouTUBE March 24 2016 na hadi March 28 2016 ilikua imetazamwa kwa zaidi ya mara laki moja na elfu hamsini na tano (155, 066). 
Kwa sasa hivi Wasanii wengi wa Afrika ni jambo la kushukuru na kufurahi pale wanapoona video zao zikichezwa kwenye kituo kikubwa cha TV kama hiki ambacho iliripotiwa kila mwezi huzikatalia video za Wasanii wengine ambazo zimeshindwa kufikia kiwango cha ubora kinachotakiwa kuanzia kwenye video mpaka audio.

Kama ulilikosa goli la Samatta lililoipa Taifa Stars point tatu dhidi ya Chad March 23 2016 (+Video)


March 23 2016 Taifa Srars ilicheza na Chad katika uwanja wa Idriss Mahamat Chad, Taifa Stars ikiwa ugenini, ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta dakika ya 30 baada ya kupokea krosi safi kutoka kwa Farid Musa.
Unaweza licheki hapa chini

VideoMPYA: Vanessa Mdee katuletea hii mpya inaitwa ‘niroge’

Itazame hapo chine Video ya Vanesa Mdee inaitwa "NIROGE"
 

Tazam apicha za Diamond, Mama yake, Zari na Tiffah wakila bata nchini Sweden #FromTandaleToTheWorldTour

Mwanamuziki mkongwe wa muziki wa Bongo fleva,Diamond Platnumz, Baada ya kumaliza tour za hapa nchini kuusambaza wimbo wa Kwetu aliouimba msanii mpya katika label ya Wasafi ameamua kuichukua familia yake akiwemo Mama yake mzazi, Zari na Tiffah ambaye ni mtoto wake pamoja na member wengine wa Wasafi akufanya tour ulimwenguni waliyo iita #FromTandaleToTheWorldTour.




Matokeo ya Rais Zanzibar yemetangazwa hizi ni picha kutoka eneo la tukio

Leo March 21 Tume ya Uchaguzu Zanzibar imetangaza matokeo ya uchaguzi ambapo imemtangaza mgombea wa CCM Dk Ali Mohamed Shein kuwa Rais Mteule wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuibuka na ushindi wa asilimia 91.4%.
Nimekuwekea Picha 15 za Matukio mbalimbali wakati wa utangazaji wa matokeo.




Paul Makonda katangaza donge la Mil moja , majambazi wahusishwa ndani..

Leo March 18 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amekutana na Kamanda wa Polisi kanda maalum Simon Sirro pamoja na Askari Polisi kwa lengo la kujionea mwenendo wa jeshi hilo, lakini kubwa ni hili la kutangaza kutoa zawadi ya milioni moja kila baad ya miezi mitatu kwa kila Askari Polisi aliyepambana na majambazi.
Askari wetu wanafanya kazi katika mzangira magumu na wanachangamoto kubwa, lakini nimeona nitengeneze mfumo wa kuwapa motisha, kwahiyo nimeongea na Kamanda Sirro nimemuambia kuwa kila askari atakayeonekana amefanya vizuri mimi kama mkuu wa mkoa nitakuwa na zawadi ya milioni moja kwake kama motisha‘ ;-Paul Makonda
Kuna watu wengi wana silaha halali na wawengine wanamiliki isivyo halali, kwahiyo tumekubaliana kuanzia leo hadi tarehe 1 aprili 2016 tunawaomba wana Dar es salaam wote waende kwenye ofisi za polisi kutoa taarifa za uhalali wa silaha zao, tunataka kujihakikishia tunzao silaha ngapi katika mkoa wetu kwamaana kuna wengine wanazitumia kinyume cha taratibu’ ;-Paul Makonda
Sasa olewako tukukute unamiliki silaha, tunahitaji kuliona jiji letu la Dar es salaam linaongoza kwa amani, hatutaki kuona majambazi wakipora kwenye mabenki wala kuwapora watu kwa silaha‘ ;-Paul Makonda
Ilikupita hii Video ya Agizo la kwanza alilolitoa Paul Makonda kama mkuu wa mkoa?


Video Behind the Scene ya Harmonize ft Diamond Platinumz

WCB Wasafi wameachia behind the Scene ya video ya wimbo Bado wa Harmonize aliyomshirikisha Diamond. Katika video hiyo moja ya tukio kubwa ni lile ambao linaonyesha jinsi uongozi wa Harmonize ulivyokaliwa kooni baada ya Harmonize kuanguka na pikipiki na kuiharibu.

Video: Sauti Sol Ft Alikiba - Unconditionally Bae

Sauti Sol (Kenya) and Alikiba (Tanzania) release UNCONDITIONALLY BAE, a danceable love ballad. In the song, Sauti Sol and Alikiba sing about the difficulty of finding love in the modern day world. The music video is poised to unite fans across East Africa and Africa at large, through dance and its strong message. #SautiSolAlikiba #UnconditionallyBae

FULL VIDEO: Mwanzo mwisho Lulu alivyoitembeza tuzo

March 8 2016  ilikuwa ni zamu ya Elizabeth Michael ‘Lulu’ nyumbani na tuzo yake ya filamu bora ya Afrika Mashariki, kamera ya AYO TV ilibahatika kuyakamata matukio yote makubwa yaliyohappen katika ujio huo kuanzia uwanja wa ndege hadi katika viwanja vya  Escape one Dar es salaam, pia watanzania walivyojitokeza kuipokea tuzo hiyo ya Africa Magic Viewer’s Choice Awards2016.
Hii hapa full video….

 

VIDEO:Watanzania Richie na Lulu walivyoshinda tuzo Nigeria


Jumamosi ya March 5 2016 Waigizaji wawili wa Tanzania walishinda tuzo kwenye tukio la Africa Magic Viewer’s choice Awards 2016 huko Lagos Nigeria ambao ni Single Mtambalike ‘Richie’ na Elizabeth MichaelLulu’

Picha: Mapokezi ya Lulu Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam

Picha za mapokezi za Mshindi wa Tuzo ya AMVCA2016 kipengele cha Movie bora ya Afrika Mashariki elizabeth michael ‘Lulu’ wakati akiwasili kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Dar es Salaam (JNIA) akitokea Nigeria.



VIDEO: Mtazame huyu anaeigilizia sauti ya J.Kikwete na Dr. Magufuli Je kawapatia?


Kuna watu wanaweza kuigiza sauti ya mtu alafu ukiwasikiliza unacheka na kubaki mdomo wazi… huyu jamaa ni miongoni mwa hao Mamaster, mtazame anaitwa Shaphii Omary kwenye hii video hapo chini
 
KUTANA NA HUYU MCHEKESHAJI MWENGINE ALIYEIIGILIZIA SAUTI YA RAIS MAGUFULI…. JINA LAKE NI MLUGALUGA, MTAZAME KWENYE HII VIDEO HAPA CHINI.



 

Harmonize azungumza kuhusu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Huddah

Harmonize azungumza kuhusu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanadada Huddah 

 Harmonize alikanusha kuwepo kwa mahusiano yake na mwanadada huyo japokuwa walisha wahi kukutana katika harakati za kufanya kazi lakini hawana mahusiano ya kimapenzi. Amesema kuwa Huddah ni miongoni mwa wanawake wazuri lakini sio kweli kuwa wanamahusiano ya kimapenzi bali wana project ya pamoja ambayo wanatarajia kuifanya siku za karibuni.

Lakini kipindi cha nyuma wawili hawa walionekana kwenye video ya pamoja wakiwa wanapigana mabusu huku Huddah akionyesha na kusema anahisi aibu.

 

 



Diamond kakutana na Kanye West Marekani

Diamond alisafiri kuelekea Marekani Las Vegas kwa ajili ya kufanya  show, ambapo kwenye maelezo ya hii picha, ilionekana wakati huo alikuwa Los Angeles.
 Diamond anakuwa mtanzania mwingine, aliyepiga picha na Kanye West, ambapo Vanessa Mdee amewahi kukutana na Kanye West na kuongea nae.
                  Hapa ni Vanessa Mdee kulia alipokutana na Kanye West

Baada ya Kudaiwa Kumdiss Diamond Platnumz, Belle 9 Kayaandika Haya…!

Ni masaa machachetu tangu kusambaa kwa ujumbe ulioandikwa kupitia Instagram account ya staa wa bongo fleva Belle 9 ikionyesha kumdiss staa mwenzake bongoflevani Diamond Platnumz, ujumbe wenyewe ulisomeka hivi>>>

 
#Samaqhani ndugu watanzania kwa usumbufu uliojitokeza ,samahani sana kwa mwanamuziki mwenzangu@Diamondplatnumz #emailmnayoiona hapo juu ndio ya hacker aliekua anapost na kutukana watu ,tunaenda kureport na kama kuna mtu anaweza kutusaidia kuitrack hii email tunamuomba msaada wake…..asante sana @Kingkapita@kapitatechnologylimited kwa kunisaidia kurudisha account yangu #Mungu akubariki #polesana kwa niliowakwaza

Video: AY alivyo kutana na TCRA kujadili kufungiwa kwa 'Zigo remix'

TCRA yatoa sababu za kufungiwa video ya "Zigo Remix" na pia nini cha kufanya kwa AY ili iruhusiwe tena kucheza kwenye TV.

Harmonize ataja sababu ya kumshirikisha Diamond Platnumz kwenye ngoma ya 'Bado'

 Mkali wa wimbo wa ‘Aiyola’ na ‘Kidonda Changu’, Harmonize, amezidi kumng’ang’ania mkali wa Bongo Fleva Afrika Mashariki, Nasib Abdul ‘Diamond Platnumz’ kwa kuendelea kumshirikisha katika wimbo wake mpya wa ‘Bado’.

Harmonize alisema ameamua kumshirikisha mkali huyo kutokana na maoni ya mashabiki wao kufananisha uimbaji wao, hivyo wameamua kuimba pamoja ili mashabiki wao waone utofauti wao.

Beat ya wimbo huo imetengenezwa na prodyuza Fraga ambaye awali alimtumia midundo mitatu tofauti akachagua huo.

Pia video ya wimbo huu imefanyika nchini Afrika Kusini na muongozaji ni Nick, aliyeongoza video ya Aiyola ya Harmonize, ‘Make Me Sing’ ya Aka na Diamond, ‘Love Boat’ ya Kcee na Diamond na ‘Walk it off’ ya Fid Q.
TAZAMA VIDEO

Disqus Shortname

Comments system